Maradhi ya moyo ikiwemo shinikizo la damu ni miongoni mwa magonjwa yanayoongezeka kwa kasi
ulimwenguni kote ikiwemo Zanzibar.
Z-NCDA inajumuika na wananchi wote kuadhimisha siku hii kwa kutoa elimu juu ya namna ya
kujikinga na maradhi hayo kwani kwa asilima kubwa maradhi haya yanaweza kuepukika.
Ujumbe wa mwak huu unasema:
Uweke moyo wako katika hali ya Afya popote pale ulipo. Ujumbe huu unasisitiza kuwa kila mtu
achukue jukumu la kuutunza moyo wake popote pale alipo, mfano anapokuwa maeneo ya
kazi,nyumbani,sehemu za starehe nk, ahakikishe anaipuka mambo yote ambayo yanapelekea moyo
wake kuugua.
Kama kuepuka kula mlo usiokamili ikiwemo matumizi makubwa ya vyakula vya uwanga,
vyakula vyenye mafuta kwa wingi na chumvi nyingi, epuka kutumia vilevi,
epuka kutumia tumbaku ikiwemo kuvuta sigara, fanya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku.